Kitalinga-Bwisi (lugha)

Kitalinga-Bwisi (pia Lubwisi) ni lugha ya Kibantu nchini Uganda inayozungumzwa na Wabwisi. Mwaka wa 2002 idadi ya wasemaji wa Kitalinga-Bwisi nchini Uganda imehesabiwa kuwa watu 68,500. Pia kuna wasemaji kama 30,000 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kitalinga-Bwisi iko katika kundi la J20.


From Wikipedia, the free encyclopedia ยท View on Wikipedia

Developed by Tubidy